IGP Sirro aagiza kukamatwa kwa wafanyabiashara wakwepa kodi

0
63

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ameagiza wafanyabiashara na watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi nchini kuchukuliwa hatua kali kwani wanarudisha nyuma na kuchelewesha maendeleo ya nchi.

IGP Sirro amesema hayo jana alipofanya ziara mkoani Mbeya na kuwaagiza askari wa vikosi mbalimbali vya polisi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi.

Sirro amesema kuwa “Kuna watu wanafikiri ni sifa kufanya magendo wote tunajua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyo tumepanga mpango mkakati wa kuwashughulikia vizuri sana wale ambao wanakwepa kulipa kodi, wananchi wetu wanapaswa kubadilisha mtazamo wao waone wanawajibika kwenye kulipa kodi sababu kodi ndiyo inafanya maendeleo ya nchi yetu.

Pia ameendelea kusema kuwa kodi ndiyo inaleta madawa, kodi inaleta barabara na kodi ndiyo kila kitu. Na wale ambao wanakwepa kulipa kodi nimetoa maelekezo kuwashughulikia kila mahali na kila siku wanasikia Amiri Jeshi Mkuu anazungumzia habari hii sasa wewe unayekwepa kulipa kodi ni nani”.

IGP Sirro aliwataka wafanyabiashara pamoja na wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele zaidi.

LEAVE A REPLY