Iggy Azalea akanusha kutoka kimapenzi na French Montana

0
155

Rapper kutoka Australia, Iggy Azalea amekanusha uvumi ulioenea kwamba ana mahusiano ya kimapenzi na staa wa Hip-Hop nchini Marekani, French Montana.

Wawili hao walionekana pamoja katika jiji la Las Vegas, walikohudhuria show ya mwanamuziki, Jennifer Lopez, Caesar’s Palace na kisha kukaa pamoja hadi show hiyo ilipoisha.

Wakati ambapo wengi walihisi kuwa wawili hao walikuwa wakielekea kuwa na uhusiano wa kimapenzi, Iggy amekanusha tetesi hizo wakati akihojiwa kwenye E News kwenye hafla ya 2016 Maxim Hot 100 mwishoni mwa wiki.

Mwezi uliopita Iggy alitangaza kuachana na mpenzi wake, Nick Young baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili.

Alimtuhumu Nick Young kwa kumpa mimba mama wa mtoto wake wa kiume.

LEAVE A REPLY