Idris Sultan kumbe aliwahi kumpa mimba Wema Sepetu

0
297

Mchekeshaji maarufu Bongo, Idris Sultan amefunguka na kuwa alifanikiwa kumpatia ujauzito Wema Sepetu tena wa watoto wawili lakini kwa bahati mbaya uliharibika.

Muigizaji huyo amesema kuwa ni kweli kweli alimpa mimba Wema na ni kweli kwamba ilikuwa ni mimba ya watoto mapacha hivyo haikuwa kiki na kweli  alikuwa kwenye mahusiano naye kwa takribani miaka miwili.

Mbali na hilo Idris Sultan amedai baadaye aliamua kumuacha mwanadada huyo kutokana na mambo mbalimbali ambayo alimtendea na kuamua kusonga mbele na maisha yake binafsi

Pia amesema kuwa tangu amekuwa maarufu hajawahi kuachwa ila kabla ya umaarufu ameachwa mara tatu kwenye mahusiano hivyo Wema Sepetu yeye ndiyo alimuacha.

LEAVE A REPLY