Ibrahimovich asaini mkataba mpya Manchester United

0
123

Klabu ya Manchester United imemuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja mshambuliaji wake, Zlatan Ibrahimovic.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameichezea timu hiyo michezo 46 na kushinda magoli 28 msimu uliopita na kuisadia Manchester United kushinda mataji ya Ngao ya Hisani, Eropa Ligi na kombe la Ligi (EFL).

Manchester United walitangaza kumuacha mchezaji huyo mwezi Juni baada ya kuumia msimu uliopita na angeweza kupona mwezi Desemba mwaka huu.

Kwa upande wa kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho amesema kuwa wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kutokana na mchango wake msimu uliopita na kuwasaidia kutwaa makombe matatu msimu uliopita.

Naye Ibrahimovic baada ya kusaini mkataba huo amesema kuwa amerudi tena kuisadia timu yake hiyo katika michuano tofauti inayoshiriki msimu huu.

LEAVE A REPLY