Ibrah wa Harmonize kuanza kufanya show

0
38

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrah amesema kwamba, sasa umefika wakati wa mashabiki kumuoma jukwaani baada ya janga la Corona nchini kuendelea kupungua.

Licha ya kutambulishwa kipindi ambacho kilikuwa kigumu sana kutokana na janga hilo lakini bado amekiri kuwa EP yake “STEPS” imepata mafanikio makubwa na imempa mwangaza mzuri wa safari yake ya muziki.

Ibraah kwa kushirikiana na uongozi wake wameendelea kupokea maombi ya shows na pindi hali itakapokuwa shwari basi tutarajie kumuona jukwaani.

Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva anfanya vizuri kwenye game la muziki toka atambulishwe na boss wake Harmonize kama msanii wa kwanza wa Konde Gang.

LEAVE A REPLY