Ibrah amshukuru Harmonize kumtoa kimuziki

0
46

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibraah kutoka Konde Gang amemshukuru bosi wake Harmonize kuanzia kumtoa kimuziki hadi alipompa zawadi ya gari.

Msanii huyo ambaye ni kwanza kusainiwa chini ya Konde Gang amesema kuwa yeye ndiyo mtu wa kwanza kwao kumiliki gari baada ya kupewa na boss wake huyo wa muziki wake.

Amesema kuwa yeye ni mtoto kutoka familia ya kimasikini kwani ameishia shule ya msingi na kuanza kuingia mtaani kuanza kuuza CD hivyo kusainiwa kwenye lebo hiyo ni hatua kubwa sana kwake na familia yake.

Ameendelea kusema kuwa baada ya kuchoka kuuza CD alianza kuuza makoti ya mitumba hadi siku moja mojamba wake aitwae Duke aliponiambia Harmonize anapatikana maeneo ya Kijuweni.

“Nimehangaika sana na nilitamani sana kutoboa na nimsaidie mama yangu huku mjomba wake akiniambia nisikate tamaa.

Ameongeza kusema kuwa “Kwa mara ya kwanza kuonana na Harmonize nilitetemeka sana na sikuweza kuimba vizuri, lakini alinisisitiza niimbe na nilipoimba akasema ninaweza, lakini siyo yeye wa kunisaidia bali nimuombe Mungu.”

LEAVE A REPLY