Hukumu ya Pistorius kupitiwa upya?

0
143

Mamlaka ya taifa ya waendesha mashtaka ya Afrika Kusini imetangaza nia ya kukata rufaa kupinga adhabu ‘kiduchu’ aliyopewa mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo, Oscar Pistorius kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Oscar Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya mawakili wa Steenkamp kupinga adhabu ya mwanzo ya kifungo cha miaka mitano huku akiruhusiwa kutumikia miaka minne nja ya gereza.

Mamlaka hiyo ya undeshaji mashtaka imeiita adhabu hiyo mpya kuwa ‘kukiukwa kwa haki na kunaweza kupelekea mfumo wa sheria kudharauliwa na wananchi’

Taarifa ya mamlaka hiyo iliyotolewa jana imenukuliwa ikidai kuwa ‘adhabu aliyopewa Pistorius haiendani na ukubwa wa kosa la mauaji alilolitenda na ni adhabu ndogo mno na inastua’.

Jaji Thokozile Masipa aliyetoa hukumu hiyo amedai kuwa adhabu kwa Pistorius ilitakiwa iwe ya haki kwa Pistorius na kwa familia ya marehemu.

‘Kifungo cha muda mrefu kisingesaidia haki, maoni ya umma yanaweza kuwa na sauti kubwa na endelevu lakini hayawezi kuwa na uzito kwenye maamuzi ya mahakama hii’ alinukuliwa jaji, Masipa.

Pistorius alimpiga risasi mara nne mpenzi wake kwenye choo kilichokuwa kimefungwa kwa ndani kwenye nyumba yake iliyopo kwenye mji wa Pretoria mwaka 2013.

LEAVE A REPLY