Hukumu ya Masogange kutolewa Februari 21

0
123

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 21, 2018 itatoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Video Queen Bongo, Agnes Gerald maarufu kama Masogange.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe kujitetea.

Akiongozwa na Mawakili Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza kutoa utetezi wake leo Masogange ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.

Masogange  anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Alidai kuwa Februari 14,2017 polisi walienda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.

LEAVE A REPLY