Huku nchi ikiwa katika hali ya hatari: Majenerali wawili wa jeshi wajiuzuru kuipinga serikali Uturuki

0
88
Mtikisiko wa hali ya kiusalama nchini Uturuki huenda ukachukua sura mpya baada ya chombo cha habari cha Al Jazeera kuripoti kuwa majenerali wawili wa jeshi la nchi hiyo wamejiuzuru kupinga hatua ya serikali ya kuendelea kukamata watu na kufungia vyombo vya habari kufuatia jaribio la kupinduliwa kwa serikali.
Kwa mujibu wa Al Jazeera majenerali hao wamejiuzuru nyadhifa za kuwa wajumbe wa baraza kuu la kijeshi la nchi hiyo muda mfupi kabla ya kikao cha baraza hilo kujadili utaratibu wa kufuata ili kufanya mabadiliko makubwa ndani ya jeshi.
Inasemekana kuwa majenerali hao wanapinga hatua ya serikali ya kutumia nguvu kuondokana na hisia za mapinduzi zilizosababishwa na jaribio la mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Julai 15.
Mpaka sasa serikali ya Uturuki tayari imeshawafuta kazi zaidi ya maafisa wa jeshi 1,223 wakiwemo majenerali 87.
Pia, serikali imevifungia vyombo vya habari kadhaa ikiwemo televisheni 16 na mashirika matatu ya habari ambayo yanadaiwa kumuunga mkono Fethullah Gulen anayelaumiwa kwa jaribio la mapinduzi hayo.

LEAVE A REPLY