Hotel ya Blue Pearl yafungwa kwa kudaiwa kodi ya pango

0
237

Kampuni ya Udalali ya Yono imeifunga Hotel ya Blue Pearl  iliyopo katika jengo la Ubungo Plaza kwa kudaiwa kodi ya Pango.

Shughuli ya kufunga hotel hiyo imefanyika leo Novemba  9 asubuhi saa 12 huku wateja waliokuwa bado wamelala wakilazimika kuamshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela amesema hotel hiyo inadaiwa kodi ya pango na Ubungo Plaza Sh.5.7 bilioni.

“Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi,” amesema Kevela

Mmoja wa wateja, Masoud Masoud akiwa na familia yake amesema”nimetoa hela nyingi na ilikuwa nikae kama wiki mbili na nimeingia jana, huu ni usumbufu.”

LEAVE A REPLY