Hivi ndivyo Diamond Platnumz ‘alivyofunika kitaifa na kimataifa’ 2016

0
1040

Huku mwaka 2016 ukielea ukingoni, Diamond Platnumz ndiye staa wa Bongo Fleva ambaye mpaka sasa ameonekana kutoa mchango mkubwa kwenye mafanikio ya mastaa wenzake ndani na nje ya Tanzania.

Hebu tazama ushahidi huu:

  1. Ngoma aliyoshirikishwa na Rich Mavoko KOKORO iko namba 2 kwenye Top 5 ya Afro Boss Airlines ya BBC 1 Extra.
  1. Salome ndiyo ngoma iliyotazamwa zaidi YOUTUBE nchini Kenya kwa mujibu wa BBC na imemrudisha kwenye chati Saida Kalori.
  1. Mastaa pacha wa P-Square walitwaa tuzo nchini Nigeria kupitia collabo waliyoshirikishwa na staa Diamond Platnumz kwenye wimbo wa ‘Kidogo’.
  1. Ngoma ya collabo na staa wa Marekani, Ne -Yo ‘Marry You’ unapata ‘airtime’ kwenye redio na Televisheni nchini Marekani na kwenye baadhi ya nchi za Ulaya.
  1. Staa wa Nigeria, Davido ameweka wazi kuwa anaitumia ngoma aliyoshirikishwa na Diamond ‘Number 1 remix’ ili kujitangaza zaidi Ulaya.
  1. Salome ndio ngoma iliyokusanya views milioni 3 YouTube ndani ya wiki 1 tu na nyingi ya views hizo zimetoka nje ya Tanzania.
  1. Chege Chigunda amefurahia mafanikio ya kupata views zaidi ya milioni 1 kwenye ngoma zake kupitia collabo yake na Diamond Platnumz ya nyimbo ‘Waache waoane’.
  1. Staa wa Zimbabwe, Jay Prayzah amefanikiwa kudhinda tuzo mbili kupitia collabo yake na Diamond Platnumz ya ngoma ‘Watora Mali’.
  2. Ngoma BADO aliyoshirikishwa na Harmonize ina views milioni 9 hadi sasa tofauti na ngoma ya Aiyola yenye views milioni 4

LEAVE A REPLY