Hit ya Darassa, ‘MUZIKI’ imepotea Tanzania na kuibukia Kenya?

0
910

Ingawa imeanza kupotea kwenye masikio ya wasikilizaji wengi wa Tanzania lakini ngoma MUZIKI ya Darassa bado ni moto wa kuotea mbali.

Kama ilivyotingisha nchini Tanzania wakati ilipokuwa inatoka na sasa ukiingia kwenye viunga vya miji mikubwa ya Kenya kama Mbombasa na Nairobi, huwezi kuuliza kitu, utaambiwa ‘WEKA MUZIKI’.

Kwenye mji wa Mombasa ishu ni MUZIKI tu kila kona ukipanda MATATU watu wanasikiliza MUZIKI tu na sio dereva na kondakta ndio wanaolazimisha watu kusikiliza bali abiria wanataka ‘MUZIKI’.

Nchini Kenya redio inayobamba zaidi kwa burudani ni Citizen ambapo mashabiki wengi wanaopiga simu au kutuma meseji kwenye kuchagua nyimbo wanataka MUZIKI tu.

Kwa zaidi ya asilimia 80 ya maombi ya nyimbo redioni yanataka MUZIKI.

Wakenya wamejitambulisha sana kuwa KISWAHILI asili yake ni huko na hata Diamond Platnumz walishawahi kudai anatokea pande za kwao.

Kwa sasa ngoma hiyo imeanza kuwainua vitini mapromota wa huko huku wengi wakitafuta namna ya kukutana na Darassa na kuona namna ya kumalizana nae kwaajili ya kufanya shoo kwenye maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Watamuweza?

Wabongo wasije kuambia Darassa ni mwenyeji wa Nairobi, kisa MUZIKI!!

LEAVE A REPLY