Hissene Habre kulipa mabilioni kwa waathirika wa ukatili wake

0
95

Mahakama maalum ya Umoja wa Afrika imemuamuru kiongozi wa zamani wa serikali ya Chad, Hissene Habre kulipa fidia ya mamilioni ya dola za Marekani kwa waathirika wa makosa dhidi ya ubinadamu yaliyofanywa na serikali yake.

Mnamo mwezi Mei, Habre alikutwa na hatia ya ubakaji, utumwa wa ngono na kuamrisha mauaji wakati wa utawala wake wa miaka 8 kati ya mwaka 1982 hadi 1990.

Hissene Habre ameamriwa kuwalipa fidia waathirika wa manyanyaso hayo inayofikia hadi $34,000 (TZS 70,000,000) kila mmoja.

Uamuzi huo wa mahakama hiyo huenda ukapelekea malipo kwa zaidi ya waathirika 4,700.

Waathirika wa vitendo vya ngono ndio waliokadiriwa kupata malipo makubwa zaidi huku ndugu wa waathirika wakilipwa kidogo.

Habre alihukumiwa kifungo cha maisha kwenye hukumu ya mfano iliyomuhusisha kiongozi wa zamani wa taifa iliyofanyika Senegal kwenye mahakama iliyokuwa inaungwa mkono na Umoja wa Afrika kwa makosa dhidi ya ubinadamu.

LEAVE A REPLY