Hillary Clinton amtaja mgombea mwenza kwa ‘Twitter’

0
158

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton ameonyesha umuhimu wa teknolojia ya mawasiliano baada ya kutumia uwanja wa mtandao wa Twitter kumtaja seneta wa jimbo la Virginia, Tima Kaine kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Seneta Kaine ambaye ana uwezo mkubwa wa kuzungumza lugha ya kihispania anatajwa kama mtu sahihi wa kumsaidia Clinton kuweza kuwafikia wamarekani wenye asili ya Hispania katika kuongeza chachu ya ushindi dhidi ya mfanyabiashara maarufu na mgombea wa nafasi hiyo kwa chama cha Republican, Donald Trump.

Washauri wa Bi. Clinton wametumia zaidi ya miezi mitatu kumtafuta mtu sahihi anayeweza kuwa na ushawishi unaohitajika kwenye uchaguzi mkuu ambao hautabiriki dhidi ya Trump na gavana, Mike Pence.

Wanachama wengine ambao walidhaniwa kuwa wangechaguliwa na Bi. Clinton ni pamoja na waziri wa kazi Thomas E. Perez, Seneta Cory Booker wa New Jersey na kamanda wa zamani wa jeshi la NATO, James G. Stavridis.

Bi. Hillary Clinton anatarajia kumtangaza rasmi Seneta Kaine kuwa mgombea mwenza baadae leo kwenye kampeni zitakazofanyika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Miami.

LEAVE A REPLY