Hillary Clinton aficha majibu ya uchunguzi wa kichomi

0
199

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Hillary Clinton ameamua kuficha matokeo ya uchunuzi wa afya yake baada ya kupatwa na maradhi ya kichomi.

Inadaiwa kuwa majibu ya uchunguzi huo yanafahamika kwa familia yake na watu wake wa karibu sana.

 Bi Hillary anatajwa kuogopa kuvuja kwa majibu hayo kwa mpinzani wake Donald Trump ambaye huenda akayatumia kwenye kampeni zake na kumsaidia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Bi. Hillary alifanyiwa uchunguzi siku ya Ijumaa baada ya kukosa nguvu akiwa jukwaani wakati akihutubia wafuasi wake kabla ya kusaidiwa na walinzi wake na kukatisha ziara ya jiji la California.

Hata hivyo, baada ya kuhudhuria maadhimisho ya matukio ya kigaidi ya 9/11 na kuondoka mapema kwenye shughuli hiyo huku akidaiwa kuonekana dhaifu, Bi. Clinton alijitokeza siku ya Jumatatu na kufanya mahojiano na kituo cha CNN na kudai yuko ‘ngangari’.

Kwan upend mwingine Bi. Clinton amekiri kuupinga ushauri aliouita wa ‘hekima’ aliopewa na daktari wa kupumzika kwa siku 5 na kusema anatarajia kurejea kwenye mchakamchaka kwenye siku chache zijazo.

LEAVE A REPLY