Hiki hapa kikosi cha Simba dhidi ya waarabu leo

0
1004

Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre amepanga kikosi chake ambacho kitaanza leo kwenye mchezo wao dhidi ya Al Masry ya Misri.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa ni wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika na utaanza majira ya saa 12 jioni, ingawa Lechantre hakufura­hishwa na muda huo uliopangwa na viongozi.

Katika kikosi hicho ambacho golini yupo Aishi Manula, walinzi wake ni Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei.

Kwenye kiungo wapo; Jonas Mkude, Nicholaus Gyan, Shiza Kichuya huku washambuliaji wakiwa ni Bocco na Okwi.

LEAVE A REPLY