Hii ndiyo bei ya Zuchu ukimtaka kwenye show yako

0
79

Meneja wa Diamond Platnumz na WCB, Sallam Sk amefunguka na kusema kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya kwa Zuchu, promota akimtaka muimbaji huyo dau lake ni Tsh milioni 20.

Sallam amedai muimbaji huyo hana hata mwaka kwenye muziki lakini uwekezaji walioufanya ni mkubwa kuliko wasanii wengine ndani ya lebo hiyo ya WCB.

Zuchu ni mwanamuziki wa pili wa kike kujiunga na lebo ya WCB baada ya Queen Darlin ambapo toka ajiunge na lebo hiyo amekuwa akifanya vizuri kutokana na nyimbo zake kupenda na mashabiki hapa nchini.

Zuchu amekuwa miongoni mwa wasanii wachache waliokubalika zaidi kwa mashabiki na kupata mafanikio makubwa ya kimuziki ndani ya muda mfupi.

Mwanamuziki huyo alifanya show ya kufa mtu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini.

LEAVE A REPLY