Hii ndio SIRI ya ku-HIT kwa ‘Moyo Sukuma Damu’

0
599

Baada ya ngoma MOYO SUKUMA DAMU kuwaweka roho juu mastaa wa muziki nchini Kenya huku staa mmojawapo nchini humo, Nyota Ndogo akiwataka wenzake wakubali kuwa Bongo Fleva iko juu, Ditto ameamua kuweka wazi the secret behind the hit song!

Staa huyo ambaye aliwahi kuwa memba wa kundi la wasanii kutoka mkoani Morogoro la WATU PORI lililokuwa chini ya Mfalme Afande Selle kwa sasa ni msanii binafsi ambaye amehamishia makazi yake jijini Dar es Salaam.

Ditto amedai kuwa ilimlazimu kufanya utafiti kwa kuuliza maswali ya msingi kuhusiana na shighuli za kiungo MOYO kwenye mwili wa binadamu ili kujiridhisha kuwa MAPENZI hayapaswi kuhusishwa na kiungo hicho.

Ditto amedai kuwa sababu kubwa zilizomfanya afanye utafiti huo ni sense of curiosity iliyopo kwa wasikilizaji ambao hufuatilia nyimbo hatua kwa hatua na neno kwa neno ili kupata kile wanachoamini wanastahili kukipata.

Je, kupenda ni kazi ya kiungo gani mwilini endapo moyo kazi yake ni kusukuma damu?

LEAVE A REPLY