Hii ndio ‘BIG DREAM’ ya Mkubwa Said Fella. Unaweza kuishinda?

0
659

Sijui wewe ‘vision’ yako ikoje? Sijui una muono gani juu yako na kile unachotamani kukitimiza kwa miaka ijayo?

Lakini meneja wa TMK Wanaume, Said Fella a.k.a Mkubwa Fella yeye ana ndoto ambayo anataka kuitimiza mwaka 2040.

Wakati akitarajia kutimiza umri wa miaka 60 ifikapo 2040 Mkubwa Fella anaamini utakuwa wakati muafaka sana kwa yeye kuwaongoza watanzania wote akiwa kama rais wa nchi hii.

Ndio Mkubwa Fella anatamani kuwania urais ifikapo mwaka 2040. Ifikapo mwaka 2040 unataka kuwa nani?

Fella anataka kuwa rais wa nchi Tanzania.

Fella ambaye taasisi yake ya Mkubwa na Wanawe inawasiamamia wasanii wapatao 102 huku kukiwa na makundi mbalimbali ya muziki yakiwemo WANAUME TMK, YAMOTO BAND, SALAM TMK, WASWAHILI TIKATIKA nk anaamini kuwa uzoefu anaoupata kwa kuwaongoza vijana hao pamoja na wananchi wa kata ya Kilungule kupitia nafasi yake ya udiwani ni uzoefu utakaomsaidia kuwaongoza watanzania.

Fella pia anashawishiwa na ushindi wake wa 89% wa kura za udiwani ambazo zimemfanya kuwa diwani aliyechaguliwa kwa kura nyingi zaidi katika mkoa wa Dar es Salaam kuwa unadhihirisha namna anavyokubalika.

Said Fella pamoja na kuongoza makundi hayo pia ni meneja mwenza wa staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz pamoja na kuwa mdau wa lebo ya WCB.

Urais kwa Fella 2040 utapatikana?

LEAVE A REPLY