Hemed PHD akanusha kujichubua

0
38

Muigizaji na msanii wa Bongo Fleva, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’ amefunguka na kusema kuwa ameshangazwa na baadhi ya watu wanaosema kuwa anajichubua wakati anapaka poda tu.

 

Hemed amewafunga midomo baadhi ya watu wanaomsema kwamba anapaka mkorogo kwa kuwaambia yeye ni mtu wa kupiga poda pekee.

 

Hemedy amesema kuwa kwenye maisha yake hajawahi kujichubua rangi aliyonayo amebarikiwa na Mungu lakini kuhusiana na poda hakatai, anapaka sana.“

 

Amesema kuwa watu wamekazana kwamba ninajichubua, naweza nikawapeleka chumbani kwangu wakakague huo mkorogo kama upo, hii ni rangi niliyojaliwa na Muumbaji, kuhusiana na poda sikatai napaka sana ndiyo maana napendwa na watoto wazuri,”.

LEAVE A REPLY