HATMA YA POGBA JULAI 31

0
544

Wakala wa mchezaji Paul Pogba, Mino Raiola amepanga tarehe ya mwisho ya kuamua mustakabali wa mchezaji huyo kuwa mwisho wa mwezi huu huku Madrid wakianza kutilia shaka thamani ya mchezaji huyo ikilinganishwa na kiwango alichokionyesha kwenye michuano ya Euro iliyomalizika kwa Ufaransa kufungwa 1-0 kwenye mechi ya fainali.

Makocha wa Real Madrid, Zidane na Jose Mourinho wa Manchester United wanavutiwa na mchezaji huyo huku kila mmoja akitaka kumalizana nae kabla ya muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili, mwishoni mwa mwezi Agosti.

pogba 3

Thamani ya Pogba imepanda kwa haraka hadi €120m baada ya miamba mikubwa ya Ulaya kuonyesha nia ya dhati ya kuipata sahihi yake.

Kwa sasa, Pogba yuko nchini Marekani kwenye mapumziko huku akiwasiliana kwa karibu na wakala wake ili kujua mustakabali wake.

Wapi? Paul Pogba ataijua hatma yake mwishoni kwa mwezi wa Julai
Wapi? Paul Pogba ataijua hatma yake mwishoni kwa mwezi wa Julai

LEAVE A REPLY