Hat-trick ya Ronaldo yaiangamiza Atletico Madrid Bernabeu

0
134

Cristiano Ronaldo ameiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu jana.

Mshambuliaji huyo raia wa Ureno alishinda bao la kwanza katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kufanya matokeo kuwa 1-0 mpaka kiindi cha kwanza kinamalizika.

Goli la pili alishnda dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha pili.

Na hii leo inatarajiwa kupigwa nusu fainali nyingine kati ya Fc Monaco dhidi ya Juventus huko Stade Louis jijini Monaco.

Na wakati huo huo Mshambuliaji nyota wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

LEAVE A REPLY