Haruna Ramadhani Shamte asaini mkataba mpya Mbeya

0
261

Beki wa pembeni wa Klabu ya Mbeya City, Haruna Ramadhani Shamte amesaini mkataba mpya ili kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya.

Klabu hiyo inayonolewa na kocha Kinnah Phiri kutoka Malawi imepania kuimalisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara unaotgemewa kuanza Agosti 20 mwaka huu.

Beki huyo wa kutumainiwa klabuni hapo amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo kutokana na mkataba wake wa hapo awali ulikuwa unaisha mwishoni mwa mwezi julai mwaka huu.