Harry Kane kuwakosa Manchester United kesho

0
111

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane hatoshiriki katika mechi dhidi ya Man United siku kesho baada ya kupata jeraha la goti.

Kane alifunga mabao mawili wakati Spurs ilipoishinda Liverpool 4-1 siku ya Jumapili kabla ya kutolewa katika dakika ya 88.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ndio mfungaji wa mabao anayeongoza katika ligi ya Uingereza msimu huu akiwa na mabao manane.

Kocha wa klabu hiyo amesema kuwa ”Madaktari na afisa wa matibabu walichukua uamuzi huo wa kutomweka hatarini”.

Kane amefunga mabao 13 katika mechi 12 za mashindano yote msimu huu huku Spurs ikiwa katika nafasi ya 3 katika jedwali la ligi.

Manchester United ni wa pili katika msimamo wa ligi nchini Uingereza wakiwa sawa kwa alama na Spurs tofauti ikiwa ni magori.

 

LEAVE A REPLY