Harry Kane ashinda tuzo ya mchezaji bora mwezi Disemba

0
114

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ameibuka mchezaji bora wa mwezi Disemba wa ligi ya England.

Kane amefunga jumla ya mabao nane katika michezo sita aliyocheza ukiwemo na ule wa Burnley na Southampton.

Kwa kutwaa tuzo hiyo sasa anakuwa sawa na kiungo wazamani wa Liverpool na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard.

Kane amesema kuwa anajisikia furaha kutwaa tuzo hiyo na atahakikisha anafanya vema katika mchezo wao ujao wikiendi hii dhidi ya Everton.

Miongoni mwa wachezaji waliyokuwa wakiwania tuzo hiyo ya mwezi Disemba ni pamoja na winga wa Chelsea, Marcos Alonso, Marko Arnautovic, Roberto Firmino na Mohamed Salah, Jesse Lingard wa Manchester United, Riyad Mahrez na beki wa Manchester City, Nicolas Otamendi.

LEAVE A REPLY