Harry Kane aingia kwenye orodha ya wafungaji bora Uingereza

0
176

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane ameingia katika orodha ya wachezaji ambao wamefunga magoli 100 na kuendelea katika ligi kuu ya Uingereza.

Kane ambaye jana  alifunga bao moja katika mchezo ambao Spurs ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Liverpool, ameingia katika orodha hiyo baada ya kufikisha magoli 100 kati ya mechi 141 aliyochezea timu hiyo.

Katika orodha hiyo Kane anashika nafasi ya 26, wakati nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Alan Shearer, ambaye alifunga magoli 260 katika ligi hiyo kabla haja staafu.

Katika magoli hayo 100 aliyofunga Kane, mabao 26 amefunga kwa mguu wa kushoto na mengine 60 amefunga kwa mguu wake wa kulia. Wakati huo huo mabao mengine 14 amefunga kwa kichwa.

LEAVE A REPLY