Harmorapa ndiye staa aliyewafunika Diamond na Ali Kiba?

0
1021

Unaweza usiamini hili lakini staa wa Hip Hop, Fid Q yeye anaamini kuwa msanii mpya wa Bongo Fleva, Harmorapa ndiye msanii aliyewatoa kwa knock-out mastaa wakubwa akiwemo Diamond na Ali Kiba.

Fid Q anaamini kuwa hakuna staa wa Bongo ambaye kwa leo anahesabika kama international brand ambaye aliweza kujitangaza kabla ya kutoa kazi ya maana ya muziki.

Fid Q amesifia SHOWBIZ iliyofanywa na management ya Harmorapa na kudai imeweza kumuweka msanii huyo kwenye ramani hata kabla hajasifiwa kwa ngoma zake.

Je, ataweza kulinda hadhi hiyo? Ni swali ambalo anapaswa kulijibu mwenyewe kwa kupitia kazi atakazozifanya.

LEAVE A REPLY