Harmorapa akanusha kupokea malipo ya dili la kinywaji cha swala

0
72

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Harmorapa amedai kuwa hajapokea pesa yoyote katika dili la kinywaji cha Swala tokea alipotangazwa Machi 26 mwaka 2017 kuwa balozi wa kinywaji hicho.

Harmorapa amedai kuwa hata yeye amesikia tetesi tu kuwa alilipwa milioni 100 licha ya kuwa hajapokea pesa hizo.

Kuhusu dili la kinywa cha Swala msanii huo akafunguka “Kiujumla niseme tu kwamba baadae mimi nikaona sielewi elewi inakuaje kuwaje maana kulikuwa na maneno mengi mengi vitu vikawa haviendi  nikajiuliza kuna nini na nikaona tu niyamaze ni kaushe maana sijui chochote kinachoendelea.”

Pia amesema kuwa  Nilikuwa tu naona maneno maneno mtandaoni kuwa Harmorapa amesainiwa kwa dili la milioni 100 sijui nini , nikashangaa kuona mbona mimi sina hata kiasi hicho ambacho kinatajwa tajwa mitandaoni mwisho wa siku nikaona bora tu nikaushe.”

Ameendelea kusema kuwa kuhusu ukaribu  wake na mtayarishaji wa muziki nchini P-Funk, Harmo ameeleza kuwa yeye na Producer huyo hawana ukaribu kama mwanzo ila anamshukuru sana kwa mchango wake.

LEAVE A REPLY