Harmorapa adai atatimiza ndoto zake za kumuoa Wema Sepetu

0
192

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa amesema na amini naye ipo siku atatimiza ndoto zake na kumuoa Wema Sepetu kama alivyofanya Dogo Janja kwa Uwoya.

Kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmorapa ameandika ujumbe akisema kwamba hatokuja kukata tamaa juu ya ndoto yake ya kumng’oa ‘Tz Sweetheart’Wema Sepetu na hatimaye kumuweka ndani kama mke wake.

“Naamini sana katika ndoto kua ipo siku ndoto unayoota itatimia na kuwa kweli, sina cha kusema zaidi ya kumpa hongera Dogo Janja, naamini ushupavu na kutovunjika moyo kumemfanya leo akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake, nami sivunji imani naamini Wema Sepetu ipo siku atakua wangu, ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini, kikubwa ni kutulia na ndoto yangu na kulenga ipo siku itatimia… One day you will be mine Wema Sepetu”, ameandika Harmorapa.

Dogo Janja hivi karibuni alifunga na ndoa na muigizaji wa Bongo Movie Irene Uwoya ambapo baadhi ya watu walidhani ni kiki ya kutaka kuachia wimbo.

LEAVE A REPLY