Harmonize ‘uso kwa uso’ na Jacqueline Wolper Dar Live

0
431

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize na aliyekuwa wake Jackline Wolper wanatarajia kukutana pamoja kwenye Tamasha litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Harmoneze na Wolper watakonga nyoyo za mashabiki wao kwa burudani katika sherehe za sikukuu ya Idd pili ambapo show yao wameiita KUSINIGHT na itafanyikia ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem.

Kwenye show hiyo Wolper ndiye atakayekuwa MC huku Harmonize akitumbuiza jukwaani ambapo ameahidi kufanya show ya kipekee.

Kiiingilio cha show hiyo bei ya juu itakuwa ni tsh 10,000 na kutakuwa na viingilio vya bei ya kawaida.

Mashabiki wa wasanii hao wameombwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya Tamasha hilo litakalofanyika siku ya sikukuu ya Eid El Fitr.

LEAVE A REPLY