Harmonize na Kajala wachorana tattoo za majina yao

0
60

Baada ya kuweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize na muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja wameamua kujichora tattoo za majina yao.

Harmonize na Kajala waliweka wazi mahusiano yao kwenye sikukuu ya wapendanao ‘Valentine Day’ February 14 mwaka huu visiwani Zanzibar.

Wawili hao wameachia video na picha ikiwaonyesha wamechorana tattoo shingoni ambapo kila mmoja akichora herufi ya kwanza ya jina la mwenzie.

Tattoo ya Kajala ina kofia ya kifalme katikati kukiandikwa herufi H, na chini alama ya karata ya jembe, Harmonize yake ina kofia ya malkia katikati ikiwa na herufi K na chini alama ya karata ya kopa.

LEAVE A REPLY