Harmonize kuzindua albamu mpya Mlimani City Machi 14

0
239

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize anatarajia kuzindua albamu yake ya kwanza Manchi 14 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.

Meneja wa Harmonize, Beauty Mmary maarufu kama ‘Mjerumani’ amesema Machi 14, mwaka huu itakuwa ni siku ya historia Bongo kwani mkali huyo anakwenda kuzindua albamu yake inayokwenda kwa jina la Afro East.

Pia Meneja huyo ameendelea kusema kuwa “Ni uzinduzi ambao haujawahi kutokea Bongo, hivyo niwaombe mashabiki wa muziki wetu watufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii na wale watakaopata bahati ya kualikwa, basi tutashuhudia pamoja uzinduzi huo,” alisema Mjerumani.

Kwa upande wake Harmo, amesema anatamani watu wote wangekuwepo kwenye shoo hiyo ya uzinduzi, lakini itashindikana. Hivyo wale watakaopata nafasi, watapata kitu cha tofauti kwenye uzinduzi huo.

“Binafsi ningetamani sana kila anayesoma hii apate nafasi ya kuja pale Mlimani City hiyo tarehe 14/3/2020 ili kujionea hili balaa linaloenda kutokea kwa sababu, ila kwa kuwa ipo nje ya uwezo wangu, basi hao watu 500 watakaopata nafasi ya kupewa mialiko, watakuwa pale kwa niaba ya wote.

Albamu hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa mwanamuziki huyo toka aachane na WCB na ni kwanza toka aanze muziki huo wa Bongo Fleva.

LEAVE A REPLY