Harmonize kushoot video 100 Zanzibar

0
23

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kusema kuwa anatarajia kushoot video 100 za nyimbo zake visiwani Zanzibar baada ya taratibu kukamilika.

Harmonize yupo visiwani Zanzibar kwasasa ambapo alitumbuiza kwenye fainali za mashindano ya Mapinduzi Cup iliyowakutanisha Simba na Yanga kwenye mechi ya fainali.

Kupitia instastory yake Harmonize ameweka kipande cha video kinachoonyesha vifaa mbalimbali vya kushutia na anasikika akisema anashuti video 100 visiwani zanzibar kwaajili ya mwaka 2021.

Huenda moja kati ya video hizo itakua aliyomshirikisha mrembo Anjella ambaye amefanya naye wimbo baada ya kukutana naye na kumsaidia kimuziki.

LEAVE A REPLY