Harmonize kumtambulisha rasmi Anjella

0
73

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza kumtambulisha mwanamuziki Anjela katika lebo ya Konde Gang baada ya kumshirikisha kwenye wimbo wake wa ‘All Night’.

Harmonize ametangaza kuwa March 11,2021 ndiyo itakuwa tarehe rasmi ya kumkaribisha mrembo huyo kwenye lebo ya Konde Gang baada ya kuridhika na kipaji chake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize ameandika “CONGRATS QUEEN ANJELLA MABIBI NA MABWANA SIKU YA TATEREHE 11/3/2021 PANAPO MAJALIWA YAWEZA KUWA SIKU KUBWA KWA HUYU MALKIA WA NGUVU MTHUBUTU NA MWENYEKIPAJI NASI HATUNA BUDI KUKUUNGA MKONO NA KUMRUHUSU AFANYE ANACHOWEZA KUKIFANYA.

Pia ameendelea kwa kuandika NAMAANISHA TUONE ZAIDI KIPAJI CHAKE NA UKIZINGATIA HUU NI MWEZI HUSIKA KABISA KWA WANAWAKE WA SHOKA WOTE.

SO KUTAKUWA NA PARTY RASMI KWAJILI YA Anjella PALE PALE KIWANJA CHA NYUMBANI Konde Gang KUANZIA SAA 2:00 USIKU RED CARPET NA TARATIBU ZOTE ZITAENDELEA SHARTI UWE UMEEALIKWA TUUU.

Mwisho amemaliza kwa kuandika YANI KWA WATAKAO BAHATIKA KUPATA CARD ZA MWALIKO DRESS CODE VAA UWEZAVYO PENDEZA UWA MAANA TUNACHUKUA FURSA HII KUZIALIKA MEDIA ZOTE …!!!!! TANZANIA NA NJE SO HAKIKISHA UMENOGA.

LEAVE A REPLY