Harmonize kufanya tamasha Novemba 28 mwaka huu

0
32

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza ujio wa Tamasha litakalofanyika Uwanja wa Uhuru November 28 mwaka huu na kushirikisha baadhi ya wasanii wa nje na ndani.

Tamasha hilo litajumuisha wasanii wa nje na ndani ya Tanzania ambapo litafanyika kwa siku tatu mfululizo katika uwanja wa Uhuru Jijin Dar es Salaam.

Harmonize amesema wasanii wote ambao wameshiriki kwenye album yake ya ‘Afro East’ watakuwepo na kutumbuiza na wengine pia ambao hawakushiriki.

Pia amesema kuwa mbali na wasanii kutumbuiza, Ma-DJ pia toka ndani na nje watapata nafasi ya kuonesha uwezo wao kwenye kuuchapa muziki mbele ya wahudhuriaji.

Ameoongeza kwa kusema kuwa hakutakuwa na kuchagua wasanii, Msanii mwenyewe atatuma ombi la kutaka kushiriki na atataja kiasi anachotaka kulipwa na masaa ambayo atataka kutumbuiza.

Tamasha la siku 3 mfululizo, likihusisha sio tu muziki bali kila aina ya burudani na utamaduni wa Kitanzania. Uwepo wa wasanii 15 wa Kimataifa katika ardhi yetu wakijumuika na wasanii wetu wa ndani kutoa burudani kwa siku tatu.

LEAVE A REPLY