Harmonize kuachia wimbo wa kwanza nje ya WCB

0
650

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameweka wazi kuachia wimbo wake wa kwanza uitwao kwa jina la ‘Uno’ chini ya lebo yake mpya Konde Music Worldwide.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo, alipost Cover ya wimbo na kuandika Woow.!!! Happy New Year 2020 Ujumbe uliohisiwa kuwa kazi hiyo huwenda ikatoka mwakani.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo ya Cover, wimbo huo umetayarishwa kwa ushirikiano wa watayarishaji wawili ambao ni producer Bonga na producer Hunter.

Hiyo itakuwa kazi yake ya kwanza toka ajitoe kwenye lebo ya WCB iliyo chini ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya kudumu nayo kwa muda mrefu.

Mwanamuziki huyo kwasasa ameanzisha lebo yake mwenyewe ambayo atakuwa anafanya nayo kazi huku akiwa na baadhi ya wasanii wake ambao wapo chini ya lebo ya Konde Music Worldwide ilioanza kazi hivi karibuni.

LEAVE A REPLY