Harmonize kuachia ngoma mpya Valentine Day

0
84

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ametangaza tarehe rasmi ya kuuachia wimbo wake ambao amemshirikisha mwanamuziki chipukizi wa Bongo Fleva, Anjella.

Harmonize ameweka wazi jina la wimbo kuwa ni “All Night” na utaachiwa siku ya wapendanao February,14, 2021 hivyo amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea ngoma hivyo.

Hii ni baada ya mashabiki kuwa na hamu kubwa ya kuusikiliza wimbo huo na kuulizia sana kuhusu collabo hiyo iliyotangazwa mwanzo mwa mwezi wa kwanza.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ” Happy New month …!!! My People’s 14/Anjella/2021 Trust me Sijawahi Kuwa Excited Kama Hivi wen it’s about DROPPING MUSIC But Trust me I can’t Wait 4 This RECORD it’s Going to Change Angella’s Life And Make Her Queen Thank You Sister Kwa Kidogo Ulichokifanya on Dat WORLDWIDE RECORD.

Harmonize alipata nafasi na kukutana na mwanamuziki huyo chipukizi na kuahidi kumsaidia kimuziki kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho.

LEAVE A REPLY