Harmonize kuachia albam mpya ‘High School’

0
35

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa anatarajia kuachia albam yake mpya iitwayo High School ambayo tayari imekamilika.

Harmonize amesema kuwa album hiyo tayari imekamilika kila kitu, anachosubiri ni kuona ratiba za wasanii wenzake kwenye label na kisha ataidondosha.

Pia amesema kuwa kitu alichofanya kwenye album yake hii ya Pili ni kutoshirikisha wasanii wa nje ya Tanzania, kama alivyofanya kwenye ‘Afro East’ ambayo ilisheheni majina mazito ya Afrika na dunia.

Harmonize amesema anataka kuwakaribisha watu kwenye Darasa lake na kuwaonesha sisi kama Watanzania na Wana Afrika Mashariki tunaweza kufanya aina yoyote ya muziki. Msikilize zaidi kwenye AUDIO hapo.

LEAVE A REPLY