Harmonize, Diamond Platnumz na Alikiba kuwania tuzo za Afrimma

0
51

Wasanii wa Bongo Fleva, Alikiba, Diamond Platnumz, Harmonize na Nandy wametajwa kuwania tuzo za Afrimma zitakazofanyika Novermba 15 mwaka huu.

Wasanii wengine waliotangazwa kuwania tuzo hiZo ni Rayvanny, Zuchu, Mbosso, Maua Sama na kundi la muziki la Navy Kenzo.

Kwenye orodha hiyo Diamond Platnumz ameng’ara kwenye vipengere vingi ambapo ametajwa kwenye vipenge hivi, Best Male East Africa, Artist Of The Year, Best Live Act, Best Collaboration, Song Of TheYear na Video Of The Year.

Huku Nandyofficial akiwa ametajwa kwenye kipengele cha Best Female EastAfrica ambapo atapambana na Zuchu, Rosa Ree na Maua Sama.

Navy Kenzo wao limetajwa kwenye kipengele cha Best African Group. Mtayarishaji wa muziki, S2kizzy ametajwa kwenye kipengele cha Music Producer Of TheYear, na Director Kenny ametajwa kwenye kipengele cha Best Video Director.

Tuzo hizo za Afrimma2020 zinatarajiwa kutolewa Novemba 15, 2020 na kura zimeshaanza kupigwa kwa ajili ya kuwapa washindi wa tuzo hizo maarufu barani Afrika.

LEAVE A REPLY