Harmonize autamani ubunge

0
74

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa mpango wake wa kugombea ubunge katika Jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara.

Harmonize amesema kuwa alijisikia furaha sana kuambiwa na Rais Magufuli kuwa anataka mwanamuziki huyo kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika mwezi Oktoba.

Pia amesema kuwa mambo mengine yanabaki kuwa chini ya kapeti, hivyo hakusema kama atagombea katika uchaguzi huyo.

Baada ya kutumbuiza katika mkutano wa hadhara mkoani Lindi, Rais Magufuli alisema kuwa anatamani kumuona Harmonize akigombea ubunge Tandahimba.

Jimbo la Tandahimba kwa sasa linaongozwa na Mbunge Katani Ahmadi Katani wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kama Harmonize atagombe na kuingia kwenye orodha ya wasanii ambao ni wabunge kama vile Joseph Haule (Profesa Jay), Joseph Mbilinyi (Sugu).

LEAVE A REPLY