Harmonize atangaza kusaini mwanamuziki nchini Burundi

0
320

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize a.k.a Konde Boy amesema kuwa msanii wa kwanza kusainiwa chini ya lebo yake ‘Konde Gang Worldwide’ atatoka nchini Burundi.

Akiwa jukwaani kwenye show iliyofanyika Machi 8 mjini Bujumbura nchini humo, Harmonize baada ya kuwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwenye show hiyo alinukuliwa katika hilo.

Msanii wa kwanza kusainiwa Konde Gang atatoka Burundi One Love.” Alisema Harmonize akiwa nchini Burundi alipoenda kufanya show nchini humo.

Hata hivyo baada ya kusema hilo, Harmonize pia aliongeza kuwa kabla ya kuondoka atafanya kolabo na wasanii wawili kutoka nchini humo.

LEAVE A REPLY