Harmonize atangaza kuachia album mpya

0
31

Baada ya kuachia album yake ya AFRO EAST mwaka huu, mkali wa muziki Bongo, Harmonize ametangaza ujio wa Album yake mpya.

Mwanamuziki huyo anayemiliki lebo ya Konde Gang amesema kuwa maandalizi ya Albam hiyo yamekamiliki hivyo mashabiki wake waka mkao wa kula kuipokea albam hiyo ya pili ndani yam waka huu.

Harmonize ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka picha na kuandika maneno “High School The Album”.

Hii itakuwa Album ya pili ya msanii huyo toka aingie kwenye kiwanda cha Muziki. Ikumbukwe kuwa Album yake ya AFRO EAST ina wasikikizaji wapatao Mil 9.5 kwenye mtandao wa Audiomack.

Harmonize ni mwanamuziki anayefany vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva kutokana na ubora wa kazi anazoziachia toka aachane na lebo ya WCB chini ya Harmonize.

LEAVE A REPLY