Harmonize amuomba msamaha Sarah

0
98

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Harmonize amemwangukia na kumuomba msamaa aliyekuwa mkewe, Sarah Michelotti raia wa Italia.

Kupitia wimbo wake mpya aliopafomu laivu kwenye bonge la shoo iliyoruka mtandaoni, Harmonize amemuomba msamaha mkewe huyo.

Mbali na wimbo huo pia ameandika; “Sorry & Sorry & Sorry. I’m sorry is the only Word I can use to the one of beautiful woman.

Alienipatia miaka (4) ya maisha yake, nami nikampatia (4) yangu, tulipitia mengi ila itoshe kusema nilizingua Sanaa

“Mpaka Mungu alipoamua kuniletea mtoto wangu wa kwanza Zuuh_konde na ndo ikawa mwisho wa safari yetu ya pamoja yeesss kuteleza kunatokea na muungwana huomba radhi ila ningeonekana mjinga zaidi ningeendelea kumficha mtoto wangu.

Love & respect and this one is for you…!!! In my next album…!!! My people run it up link on my bio @ceekvr…” Harmonize na Sarah waliachana mwaka jana kwa skendo ya usaliti.

LEAVE A REPLY