Harmonize amtoa mpenzi wake mtandaoni

0
235

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amesema kuwa kwasasa hataki mke wake Sarah ajihusishe na mitandao ya kijamii kwa kuwa anamtengeneza kuwa mke wa mfano.

Harmonize amesema pamoja na mke wake kuwa mtu wa kujichanganya sana lakini anataka kumuona ni mtu anayejiweka karibu zaidi na familia kuliko mitandao ya kijamii na mambo mengine.

“Sitokuwa naye karibu sana kwenye shoo zangu tofauti na zamani, lakini si kwamba hamtaniona naye, nataka awe malkia.

Ameongeza kusema kuwa sitaki awe na mazoea na vyombo vya habari ama na watu wengine, nataka atumie muda mwingi kunijali mimi na familia yangu,”alisema Harmonize.

Pia amesema pamoja na kutamani mke wake awe wa kitofauti lakini hawezi kumkataza kutumia muda wake kufanya mambo ya kimaendeleo kwa lengo la kujiongezea kipato kwa kuwa ni mtu wa kujituma sana.

LEAVE A REPLY