Harmonize alivyombeba Sarah mgongoni

0
1285

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize amejikuta akimbeba mgongoni mpenzi wake Sarah baada ya kushindwa kupanda Mlima Mkomaindo ulioko mkoani Mtwara.

Tukio hilo limetokea jana wakati msanii huyo akiwa mjini ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Masasi Rock Festival lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Sarah alionekana kuchoka na kushindwa kuendelea ambapo katika isiyotegemewa na wengi Harmonize ambaye ni mwenyeji wa Mtwara alimbeba mgongoni mpenzi wake.

Katika tamasha hilo kunatarajiwa kufanyika mashindano mbalimbali ikiwamo kupanda jiwe mkomaindo lenye urefu wa mita 1,800.

Tamasha hilo limeanza Juni 6 na litamalizika Juni 9 mwaka huu likiwa na lengo la kutangaza utalii wa ndani ya mkoa wa Mtwara.

LEAVE A REPLY