Harmonize alaumiwa na waandishi Kenya

0
356

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameingia kwenye lawama kubwa na waandishi wa habari nchini Kenya baada ya kukataa kujibu maswali kwenye mkutano wake.

Waandishi wa Habari nchini humo wamesema kuwa aliongea kwa dakika zisizopungua 3 na kisha kukataa kujibu maswali yanayohusu lebo yake ya zamani ya WCB.

Waandishi wamesema awali kabla ya mkutano huo, Waliambiwa na waandaji wa tukio hilo kuwa kutakuwa na mahojiano ya mmoja mmoja baada ya kumalizika kwa mkutano huo lakini haikufanyika hivyo.

Mwanamuziki huyo alifika katika ukumbi huo wa mkutano na wanahabari akiwa ameongozana na walinzi wake wanne na baadhi ya waandaaji wa mkutano huo.

Baada ya tukio hilo, Imeelezwa kuwa Harmonize alienda kwenye kipindi cha 10 over 10 kutambulisha wimbo wake wa UNO.

Waandishi wengi wamesema kuwa walistahili kuheshimiwa kama alivyowaheshimu wanahabari wa Tanzania wakati akitambulisha wimbo huo.

Harmonize alisafiri kwenda nchini Uganda kwa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya wa UNO ambao unaendelea kufanya vizuri katika media mbali mbali.

LEAVE A REPLY