Harmonize akutana na meneja wa T.I

0
274

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekutana na meneja wa wasanii maarufu nchini Marekani, Jason Geter ambaye anawasimamia T.I na Travis Scott.

Harmonize yupo nchini Marekani kwa ajili ya show katika miji mbali mbali nchini humo ambapo alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za Afrimma zilizofanyika mwanzoni mwa wiki hii.

Meneja wa Harmonize, Mr Puaz amesema kuwa wapo Marekani kupiga show kwenye baadhi ya miji mbalimbali ambapo pia wamepata nafasi ya kukutana na mameneja wa wanamuziki maarufu nchini Marekani.

Mr Puaz amesema kuwa leo amekutana na meneja Jason Geter na wamefanya mazungumzo ya kikazi huku akiwaahidi mashabiki wa Harmonize kukaa mkao wa kula.

Jason Geter  kwa sasa anawameneji wasanii wakubwa wawili nchini Marekani ambao ni TI na Travis Scott ambao wanafanya vizuri nchini Marekani.

LEAVE A REPLY