Harmonize akanusha kuvuta bangi

0
125

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amekanusha tuhuma zilizotolewa na Makonda kuhusu kuvuta Bangi ambapo amesema kuwa hajawahi kuvuta bangi hata siku moja.

Makonda alimtuhumu Harmonize  kwamba huwenda akawa anatumia bangi baada ya kuonekana akivuta sigara yenye moshi mzito katika moja ya video ambayo aliiweka mitandaoni akiwa nchini Ghana ambapo alikuwa kikazi.

Kauli ya RC Makonda aliitoa kwenye mkutano kati yake na wasanii wa Movie na muziki nchini ambapo walikutana kwa ajili ya kujadili kazi za Sanaa nchini.

Harmonize ameibuka na kukataa kabisa tetesi hizo na kusema wazi kuwa moshi ambao umeonekana kwenye video za Instagram ulikuwa moshi wa sigara na sio wa Bangi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alijibu tuhuma hizo kwa njia za utani akilihusisha na suala la Simba kufungwa goli 5 na Al Alhy ya Misri.

LEAVE A REPLY