Harmonize ajitamba kuwa na mjengo mkali kuliko wasanii wote Bongo

0
1260

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka WCB, Harmonize amesema kuwa ukimucha Diamond Platnumz yeye ndiyo msanii anayefuatia kuwa na nyumba nzuri nchini Tanzania.

Harmonize amesema kuwa nyumba yake hiyo ipo mbioni kukamilika siku zijazo ambayo ameijengea maeneo ya Madale jijini Dar es Salaam.

Pia mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa amefikia mafanikio hayo makubwa kutokana na ushauri mzuri anaopatiwa na mpenzi wake Sarah.

Katika hatua nyingine amefunguka tetesi za mpenzi wake Sarah kuwa na ujauzito na kueleza kuwa hilo halina ukweli ila kwa sasa anaweka mazingira mazuri kwa ajili ya mtoto.

Harmonize kwasasa anatamba na wimbo wake unakwenda kwa jina la ‘Kwa ngaru’ aliomshirikisha Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY