Harmonize afunguka ugumu anaokutana nao WCB

0
1656

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka WCB Harmonize amefunguka na kuelezea ugumu uliopo katika kufanya kazi kama msanii wa label ya WCB kutokana na ushindani.

Harmonize amefunguka na kuweka wazi kuwa ushindani ndani ya Label hiyo kati ya wasanii ambao wapo ndani ya Label ndio ugumu ambao upo humo.

Harmonize amesema ugumu uliopo WCB ni kila msanii ana uwezo mkubwa, hivyo kila mmoja anahakikisha anafanya kazi nzuri.

“Ugumu ni pale ambapo unafanya kazi na wasanii wote ambao ni talented, so way competion katika kurekodi ngoma kila mtu anataka kutoa ngoma yake kali kumshinda mwenzake, so ugumu unaanzia hapo“.

WCB ni Label kubwa kabisa Tanzania na inabeba wasanii wanaofanya vizuri sana, wasanii hao kama vile Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko, Mbosso na wengineo.

 

LEAVE A REPLY